Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mtenjele amefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara na Elimu inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo .
Katika ziara hiyo Mhe.Mtenjele amesisitiza kasi ya Ujenzi iongezeke ili miradi ikamilike kwa wakati ili Wananchi wapate huduma .
Miongoni mwa miradi aliyotembelea ni ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo Shule ya Msingi Michenjele na Mihambwe, Shule ya msingi Ghana sambamba na Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji .
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa