Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele amewataka Watendaji Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Kusimamia na kutekeleza viashiria vyote vya mkataba wa afua za lishe kwa wakati.
Amesema hayo Februari 5,2025 kwenye kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa afua za lishe ngazi ya Kata kwa kipindi cha robo ya Pili Oktoba - Desemba Mwaka 2024/2025 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Wilaya.
Aidha amesema kiashiria cha upatikanaji wa chakula shuleni kwa baadhi ya Kata kimekuwa hakitekelezwi kwa asilimia Mia moja ambapo amewahimiza Watendaji Kata kusimamia ili wazazi na walezi wachangie watoto wapate chakula cha pamoja shuleni.
#Tandahimba tumejipanga kazi zinae
ndelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa