*Awasistiza Kusajili na Kuhuisha taarifa za wakulima kwa Usahihi
Mkuu wa Wilaya Tandahimba Kanali Michael Mntenjele amekabidhi Vishkwambi 51 kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba huku akiwasistiza Kusajili na Kuhuisha taarifa za wakulima kwa usahihi ili kupata takwimu sahihi zitakazoisaidia Serikali katika mipango yake mbalimbali ikiwa pamoja na ugawaji wa pembejeo kwa Wakulima
Akizungumza kwenye mafunzo ya usajili na Uhuishaji wa taarifa za wakulima kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba leo Februari 18,2025 yaliyoandaliwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) amesema ili kupata taarifa sahihi wahakikishe wanakwenda mashambani lakini pia washirikiane na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wa maeneo husika.
" Rai yangu kwenu mkashirikiane na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ili mpate taarifa sahihi, mna vifaa hivi mkavitunze ,nendeni mashambani na mfanye kazi kama timu ili muweze kuwafikia wakulima wote,lengo la Serikali ni kuongeza uzalishaji wa zao la korosho," amesema DC Mntenjele
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Ndg.Chuma Mpore amesma baada ya mafunzo hayo Maafisa Ugani wataanza kusajili na kuhuisha taarifa za wakulima kwenye maeneo yao
#Tandahimba tumejipanga kazi zinaende
lea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa