Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka viongozi wa vyama vya msingi (Amcos) kutunza takwimu za ugawaji wa pembejeo kwa wakulima katika maeneo yao
Viongozi wa Amcoss Wilaya ya Tandahimba wakimsikiliza Mhe.Dc Sawala (hayupo pichani)
Ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuwasistiza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia,miongozo,taratibu ,kanuni na sheria katika kutoa huduma
Mhe.Kanali Patrick Sawala akieleza jambo kwa viongozi wa vyama vya msingi(hawapo pichani)
“Serikali imetoa pembejeo bure kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji, tendeni haki kwa wakulima gaweni pembejeo bila upendeleo, takwimu hizo mzitunze vizuri,”amesema Dc Sawala
Aidha Dc Sawala amesema serikali imeahidi kutoa mbegu za ufuta kwa wakulima ,ni wajibu wa wakulima wa Tandahimba kutumia nafasi hiyo ili kuweza kuongeza kipato kwa kulima mazao mengine ya kibiashara sambamba na wakulima kuendelea kusafisha mashamba yao
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa vyama vya msingi 133 vilivyopo Wilaya ya Tandahimba
Naye Meneja Mkuu wa Chama kikuu Tandahimba na Newala(Tanecu) ndg. Mohamed mwinguku amewasistiza viongozi wa vyama vya ushirika ambao hawajachukua vipima unyevu wafanye hivyo ili kuendelea kuipa thamani korosho ya Tandahimba
Meneja Mkuu wa Tanecu ndg.Mohamed Mwinguku akieleza jambo kwa viongozi wa Amcos
Afisa Kilimo wa Wilaya ndg.Issa Naumanga akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa wataendelea kushirikiana na amcos ili kuendelea kuongeza uzalisalishaji wa zao la Korosho ndani ya Wilaya
Afisa Kilimo Wilaya ya Tandahimba ndg.Issa Naumanga akieleza jambo kwa viongozi wa Amcos
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa