Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Benaya Kapinga amewataka wanannchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona kwa kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia Wilaya ipo karibu na nchi jirani
Akizungumza kwenye kikao cha ufunguzi wa taarifa fupi ya Ugonjwa wa Corona katika Wilaya ya Tandahimba Kaimu Dc ametoa maagizo kwa taasisi zote ambazo zipo ndani ya Halmashauri ya Tandahimba kuweka maji ya kunawia mikono tiririka ili kila anayeingia aweze kunawa mikono ikiwa ni hatua za awali za kujikinga na maambukizi
Kaimu Dc Benaya Kapinga akifungua kikao cha taarifa fupi ya Ugonjwa wa Corona Wilaya ya Tandahimba
“Kwa kupitia kikao hiki tunagiza taasisi zote ndani ya Wilaya ya Tandahimba waweke maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono kwa kila mtu atakayetaka huduma yoyote , shuleni na nyumbani yawekwe maji ili kujikinga na maambukizi haya,”amesema Kapinga
Aidha amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu pia katika nyumba za ibada sambamba na kuacha kusalimiana kwa kupeana mikono badala yake tahadhali za awali zichukuliwe hasa katika mikusanyiko ya watu
Wajumbe walioshiriki katika kikao hicho leo wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela ameeleza kuwa Halmashauri tayari imetenga fedha kwa ajili ya kuwezesha Kitengo cha afya kupata vifaa vya kupima joto la mwili hususan katika maeneo ya mipakani
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela(aliyesimama) akifafanua jambo
“Hii ni dharura nasisi tunapakana na nchi jirani kwa vile mipaka hii inapitisha raia wa kigeni kifaa cha kupima joto mwili katika mipaka yetu ni muhimu hivyo tunajitahidi kukipata kwa haraka ili kuweza kupimia wagonjwa badala ya kipimo cha kuweka kwapani kutokana na hali iliyopo sasa,”amesema Machela
Naye Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Tandahimba Dokta Antpas Swai amesema wananchi waendelee kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi ya Corona
Amesema kuwa tayari Wilaya imetenga Zahanati ya Mtegu kwa ajili ya dharura endapo atapatikana mgonjwa wa corona sambamba na maandalizi ya vifaa kwa timu ambayo itashughulikia wagonjwa hao
Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai
“Tumejiandaa tayari kama Hospital ya Wilaya tumetenga zahanati ya Mtegu kwa atakayedhibitika kuwa nao,lakini pia wale ambao tutawahisi pia tumetenga eneo nje ya Hospital ya Wilaya kwa ajili ya watakaosubiri majibu baada ya kuonesha dalili za awali,”amesema Dk Swai
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa