Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kununua mashine ya kukamua mafuta ya alizeti ili wananchi wapate huduma hiyo karibu
Ameyasema hayo leo Julai 12,2022 alipotembelea kiwanda cha kukamua alizeti kilichopo katika karakana ya matogoro kata ya Tandahimba
“Nawapongeza sana Halmasahauri kwa kutekeleza yale ambayo tuliazimia kama Serikali kwa umoja wetu na kufanikisha kufunga kiwanda ili wananchi wapate huduma hii,jitihada hizi zimeanzia kwenye kuhamasisha wananchi na shule zote kulima zao la alizeti na wamefanya hivi,kwaiyo wananchi sasa wanakuja kukamua mafuta yao katika kiwanda hiki,”amesema Dc Sawala
Aidha amesema wananchi watakuza kipato chao kwa kukamua mafuta kwa matumizi yao au wakitaka kuuza ili kukuza kipato chao lakini pia mashudu kutumia kwa ajili ya c mifugo
Naye Afisa Kilimo Ndg. Issa Naumanga amesema kuwa wakulima walete alizeti ambazo zimekauka vizuri ili zikikamuliwa kwenye mashine zitoe mafuta mengi lakini zisipokauka hazitoi mafuta mengi
“Mbegu za alizeti zinatakiwa zikauke ziwe na kiwango cha unyevu asilimia 12 hadi 9,mbegu ya alizeti iliyokauka ukiimwaga chini inatoa mlio lakini kuna kipimo cha kupima unyevu ,hivyo natoa wito wakulima kuhakikisha alizeti zimekauka vizuri ,”amesema Naumanga
Nao wananchi wameishukuru Serikali kwa kufunga mashine hiyo ambapo itawarahisishia wakulima wa alizeti kupata huduma hiyo karibu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa