Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Wakuu wa Idara na Vitengo (CMT) wametoa rai kwa fundi viongozi wa miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na Elimu kuongeza kasi ili miradi hiyo iweze kukamilika na wananchi waweze kunufaika nayo kwa wakati
Hayo wameeleza leo Juni 10,2022 ambapo wamefanya ziara ya kutembelea vituo vya afya vitatu ambavyo ni kituo cha afya Litehu,Mambamba na Mihambwe ambapo serikali ilitoa fedha awamu ya kwanza shilingi milioni 750 ambapo mradi wa ujenzi wa vituo vyote vitatu upo katika hatua za ukamilishaji
Katika awamu ya pili Serikali kuu imetoa fedha shilingi Milioni 750 kwa ajili ya kuongeza majengo katika vituo hivyo vitatu fedha ambazo tayari zimeanza kufanya kazi ambapo tayari msingi wa jengo umechimbwa
Aidha katika ziara hiyo CMT ilitembelea Shule ya Sekondari ya mfano ya Litehu ambapo jumla ya kiasi cha shilingi Milioni 470 zimetolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba nane vya madarasa,jengo la maktaba,chumba cha kompyuta,maabara ya fizikia,bailojia na kemia,jengo la utawala na ujenzi wa matundu ya vyoo 20
Miradi hiyo ikikamilika wananchi watapata huduma ya afya karibu na wanafunzi wa kata ya litehu watasoma katika kata yao ambapo kwa sasa wanasoma katika kata jirani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa