Bodi ya Mfuko wa Elimu Wilaya ya Tandahimba imefanya ziara ya kukagua Miradi Sita ya Elimu yenye zaidi ya Tsh.Milioni 270 inayotekelezwa katika Wilaya hiyo sambamba na Maendeleo ya wanafunzi katika Shule za Msingi ambapo katika ukaguzi huo Bodi hiyo imetoa wito kwa wazazi kushirikiana na walimu katika malezi ya kitaaluma kwa watoto wao.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Madarasa na Ofisi Shule ya Msingi Namitondi Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Tandahimba Bakiri Msham amesema pamoja na Serikali kuboresha miundombinu ya Elimu ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanafuatilia Maendeleo ya kitaaluma kwa watoto ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao na sio kuwaachia walimu peke yake.
Aidha, Bodi ya Mfuko wa Elimu Tandahimba imetoa fedha kiasi Cha Tsh.Milioni 104.4 Kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vinne(4) vya Madarasa, Matundu 10 ya Vyoo, Umaliziaji wa Vyumba Viwili vya Madarasa na madawati 180 ambapo Miradi hiyo inatekelezwa katika Shule za Msingi Amani, Matogoro, Mikuyu, na Likolombe.
Vilevile Bodi hiyo imepongeza Ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari Luagala lenye thamani ya Tsh. Milioni 141 lililojengwa kwa ufadhili wa TEA sambamba na Ujenzi wa Madarasa manne na Ofisi Shule ya Msingi Namit
ondi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa