Na Kitengo cha Mawasiliano
Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamefanya Uchaguzi wa Viongozi na Wajumbe wa ngazi zote wanaounda baraza hilo
Uchaguzi huo umefanyika leo Januari 13,2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ,Wajumbe wawakilishi walichaguliwa na kisha wajumbe hao walichagua Katibu na Katibu Msaidizi
Afisa Kazi Mkoa wa Mtwara Ndg.Paskali Kapinga amemtangaza Bi.Judicy Mnzava kuwa Katibu kwa kupata kura 20 na Ndg.Mruta Kamana kuwa Katibu Msaidizi baada ya kupata kura 17 ambapo jumla ya wapiga kura wote ilikuwa 37 hakuna kura iliyoharibika
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Jane Mallongo amewapongeza viongozi na wajumbe waliochaguliwa na kuwataka kufanya kazi kwa weledi sambamba na kutatua changamoto mbalimbali za wafanyakazi
Aidha Viongozi na wajumbe waliochaguliwa wameahidi kuendelea kuwa na nidhamu ya kazi kwa kuzingatia miongozo sheria na kanuni
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa