Na. Kitengo cha Mawasiliano
Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wameridhia kupitisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti kwa mwaka 2023/2024 yenye shilingi Bilioni arobaini na moja ,milioni mia tano themanini na moja na sabini na sita elfu (41,581,076,000)
Akiwasilisha rasimu ya bajeti katika kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Februari 3,2023 Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Ndg.Charles Mihayo amesema kuwa fedha hizo zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri,ruzuku kutoka Serikali Kuu,Wafadhili na michango ya jamii
Amesema kwa upande wa Halmashauri imejiwekea lengo la kukusanya shilingi 5,558,727,900 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani vya mapato
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa