-Watendaji wa Kata na Vijiji watunukiwa vyeti vya pongezi.
Baraza la wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limefanyika Leo Februari 7, 2025 Kwa ajili ya kujadili makisio ya Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Baraza hilo limeongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya David Sinyanya limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali Wakiwemo wa vyama vya wafanyakazi, pamoja na Watumishi wa Halmashauri hiyo .
Sambamba na kujadili Bajeti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba DCI.Mariam Mwanzalima amewatunuku vyeti vya pongezi watendaji wa Kata na Vijiji ikiwa ni sehemu ya kutambua Mchango wao na utenda kazi uliotukuka katika kuwahudumia Wananchi.
Aidha, katika Baraza hilo Watumishi wa Halmashauri wamesisitizwa kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ili kuleta matokeo Chanya kwa Jamii.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa