Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limemwomba Mkurugenzi Mtendaji kukamilisha taratibu ili Miji Midogo ya Tandahimba na Mahuta kuwa Miji kamili na iweze kujiendesha kiuchumi
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wakiwa kwenye kikao cha robo ya pili
Akijibu swali la papo kwa papo ambalo liliulizwa na Mheshimiwa Diwani wa Tandahimba Aidan Chipande kuhusu kuchelewa kwa wa Miji midogo ya Tandahimba na Mahuta kuwa Miji kamili Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ally Machela amesema kuwa ili miji iwe kamili taratibu,sheria na kanuni lazima zizingatiwe ambapo mchakato unaendelea
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndg Ally Machela akijibu swali la papo kwa papo
“Katika ukamilishaji wa Miji hii kuna taratibu ,sheria,kanuni na miongozo lazima izingatiwe kwaiyo tunaendelea na mchakato wa kuhakikisha zinakuwa Miji kamili ,”amesema Ndugu Machela
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amevitaka vyama vya msingi vinavyoendelea kukata shilingi elfu moja kwa wakulima wanaojihorodhesha kwa ajili ya pembejeo kuacha kwakuwa ni kinyume na utaratibu uliowekwa
Dc Waryuba akitoa ufafanuzi kwa Waheshimiwa Madiwani
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya madiwani kutoa taarifa za wananchi katika maeneo yao kuendelea kukatwa fedha ya kujioredhesha katika vyama vyao vya msingi kwa ajili ya kupewa pembejeo hivyo wakulima wengine kuacha kujiandikisha kwa kushindwa kulipa fedha hiyo
“Waheshimiwa madiwani kama ambavyo amesema mtaalamu wa Kilimo kuwa kujiandikisha ni bure mkalisimamie hilo ili wakulima wetu wajitokeze kujiandisha kama kuna chama kinaendelea na utaratibu wa kuwatoza fedha toeni taarifa sheria ichukue mkondo wake,”amesema Waryuba
Kamati ya Ulinzi na Usalama na wataalamu wa Halmashauri wakiwa kwenye Baraza la Madiwani
Katika Baraza hilo la siku mbili masuala ambayo yaliweza kujadiliwa ni pamoja na barabara,Kilimo,Pembejeo,ushirika,Elimu,Mikopo ya vijana,walemavu na wanawake kuwafikia kwa wakati
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Katani Katani akizungumzia suala la Ushirika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa