Na Kitengo cha Mawasiliano
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limewapongeza wanariadha wawili ambao walishiriki mashindano ya Shimisemita 2022 na kupata medali na cheti
Akitoa pongezi hizo katika Mkutano wa Baraza la madiwani Novemba 24,2022 uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amesema wanawapongeza kwa hatua hiyo
“Sisi Madiwani tunawapongeza sana kwa kwenda kushiriki na kurudi na medali na cheti,hongereni sana lakini pia mmetupa hamasa zaidi , mwakani tutajipanga ili tuweze kufanya vizuri zaidi,”
Katika mashindano hayo yaliyofanyika Mkoani Morogoro kuanzia Oktoba 18 hadi 31,2022 kati ya Halmashauri 46 zilizoshiriki katika mashindano ya Shimisemita Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeshika nafasi ya 10 katika ushindi wa wa jumla
Washiriki wawili ambao waliiwakilisha Halmsahauri ni Mwl Helena Mkuti ambaye alikimbia mita 100 na Mwl Gelord Sebastian ambae alikimbia mita 1500 na kushika nafasi ya tatu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa