Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepitisha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 43.7
Baraza hilo ambalo limefanyia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba limepitisha fedha hizo zilizotokana na mapato ya ruzuku kutoka serikali kuu , mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri na wafadhili
Baraza la madiwani Halmashauri ya Tandahimba wamepitisha rasimu ya bajeti
Akizungumza kwenye baraza hilo Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mh.Katani Katani amesema kuwa madiwani na wakuu wa idara washirikiane pamoja ili kuijenga Tandahimba na kuwaletea wananchi maendeleo
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mh.Katani Katani akitoa neno kwenye baraza la madiwani
“Madiwani mshirikiane na wakuu wa Idara ili kuwaletea maendeleo kwa kasi wananchi wa Tandahimba,tumechelewa tunahitaji kukimbia lakini tunategemeana hivyo msimamie miradi inayokuja katika maeneo yenu kwa uadilifu,”amesema Mh.Katani
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kuwa fedha za miradi ambazo zinakwenda kwenye kata zitumike kwa kutekeleza miradi yenye ubora kwakuwa serikali inatumia fedha nyingi kuwaletea wananchi maendeleo
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mh.Sebastian Waryuba akizungumza kwenye baraza la madiwani
“Simamieni miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu kwa kuzingatia taratibu na kanuni ili wananchi wanufaike nayo nawapongeza madiwani kwa kuipitisha bajeti ya mwaka 2021/2022 ,”amesema Dc Waryuba
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Said Msomoka amesema kuwa miradi inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali wataalaum wataendelea kusimamia ipasavyo ilete tija kwa wananchi wa Tandahimba
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba akitoa pongezi kwa idara ya mipango kwa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2021/2022
“Nawapongeza Idara ya Mipango kwa maandalizi ya bajeti hii lakini naamini wataalam wa Halmashauri wana nia ya kuifanya Tandahimba iwe juu kimaendeleo lakini pale kwenye mapungufu ofisi zipo wazi kupata ufafanuzi au kutoa ushauri kuhusu eneo lako kwakuwa wote tunaijenga Tandahimba moja kimaendeleo ,”amesema ndg Msomoka
Afisa Mipango ndg .Karim Mputa akisoma rasimu ya bajeti ya mwaka 2021/2022 kwenye baraza la madiwani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa