Na Kitengo cha Mawasiliano
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamempongeza Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha za miradi ya utekelezaji wa miundombinu ya shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kiasi Tsh.665,100,000 kupitia mradi wa BOOST
Pongezi hizo wamezitoa Mei 11,2023 wakati wakiwasilisha taarifa za miradi ya Maendeleo ya Kata zao katika mkutano wa Baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya tatu 2022/2023 uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Akifafanua zaidi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema fedha hizo tayari zimeanza kufanya kazi katika maeneo husika ambapo Halmashauri imejipanga kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na ubora
" Tunamshukuru sana Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizi ambazo zitaboresha ujifunzaji na ufundishaji katika shule zetu za msingi ,sisi Halmashauri kwa Ushirikiano tulionao tutatekeleza miradi hii kwa wakati na ubora ili iweze kutumika ," amesema Mwenyekiti
Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya tatu 2022/2023 umeanza Mei 11,2023 na utahitimishwa Mei 12,2023 ambapo agenda tatu kati ya tisa zimewasilishwa na kujadiliwa kwa siku ya kwanza
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa