Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limepitisha Makisio ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya kiasi cha Shilingi Bilioni 40.2.
Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 umewasilishwa na Mkuu wa Idara ya Mipango David Sinyanya kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri .
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imekadiria kukusanya na kutumia Shilingi Bilioni 40.2 ambapo Ruzuku ya Mishahara Silingi Bilioni 24.9, Ruzuku ya matumizi mengineyo Shilingi Bilioni 2.8,Mapato ya ndani shilingi Bilioni 7.3 na ruzuku ya wafadhili shilingi Bilioni 5.06.
Sambamba na Bajeti hiyo ya Halmashauri Taasisi mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zimewasilisha Bajeti zao katika Baraza hilo ambapo Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Tandahimba Scola Nyagali akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/2026 amesema kiasi cha Shilingii Bilioni 8.5 kimekadiriwa kutekeleza ujenzi na matengenezo ya Mtandao wa barabara .
Nyagali ameongeza kuwa kupitia bajeti hiyo TARURA itafanya matengenezo ya kawaida KM 483.57,Matengenezo ya sehemu korofi KM 105.05, Matengenezo Maalum KM 60.20,Matengenezo ya barabara kwa kiwango cha lami KM 9.19,ukarabati wa barabara KM 16,Ujenzi wa mifereji M.1200 na ujenzi wa Makalavati
Naye Mwakilishi wa Wakala wa Maji safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Tandahimba Hassan Mawenya amesema Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ni shilingi Bilioni 4.2 ambayo itatumika kwenye utekelezaji wa miradi ya Maji katika Wilaya hiyo.
Baraza la Madiwani limepongeza waandaaji wa Bajeti hiyo kwa kuzingatia vipaumbele mahususi vilivyowekwa Kwa ajili ya Maendeleo ya Halmashauri wakiamini Miradi ya Maendeleo itatekelezwa na Wananchi watapata huduma Stahiki.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa