Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepitisha rasimu ya mapendekezo ya bajeti kiasi cha shilingi 45,102,660,150 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023
Akiwasilisha bajeti hiyo leo Februari 10,2022 Mkurugenzi Mtendaji ndugu Mussa Gama katika baraza maalum la Bajeti amesema kuwa fedha hizo zinatokana na vyanzo vyake vya mapato ya ,Ruzuku kutoka Serikali kuu,Wahisani pamoja na michango ya jamii
Mkurugenzi amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 wanatarajia kukusanya mapato ya ndani zaidi ya shilingi 4,970,502,000 ambazo zinatarajia kukusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ya halmashauri
Akiendesha kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa pamoja na madiwani wameipitisha bajeti hiyo
Mwenyekiti amesema kuwa Jitihada kubwa ifanyike ili bajeti hiyo itekelezeke kwa kuhakikisha suala la ukusanyaji wa mapato katika maeneo yote yanafikiwa ili wananchi waweze kuendelea kupata maendeleo
“Bajeti hii tumeiridhia na imemgusa mwananchi moja kwa moja,kwasababu inakwenda kugusa afya elimu ,mifugo,kilimo na mengine mengi,ni matumaini yetu kuwa itatekelezeka ili wananchi waweze kuona maendeleo hayo katika maeneo yao,”amesema Mwenyekiti
Aidha madiwani kwa nyakati tofauti wameipongeza bajeti hiyo kuwa imejitahidi kugusa katika maeneo mengi hiyo itawanufaisha wananchi wa Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa