Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa kipindi cha miaka mitano limefanikiwa kupitisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo utekelezaji wa barabara ya lami ya km3 kwa mapato ya ndani na kuridhia kukatwa kwa shilingi 20 kwa kila kilo moja ya korosho kwa wakulima kwa ajili ya maendeleo ya wananchi .
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Tandahimba
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano 2015/2016 hadi mwaka 2019/2020 ambayo iliwasilishwa na Afisa Mipango Hassan Nzyungu katika Baraza la Madiwani ambalo limefanyika Katika ukumbi wa Halmashauri
“Kwa kipindi cha miaka mitano shughuli mbalimbali za maendeleo zimefanyika kwa ushirikiano mkubwa wa madiwani kama ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho,karakana ya ufundi na usimamizi wa miradi mbalimbali ambayo imefanyika katika kata ,”amesema Nzyungu
Afisa Mipango Hassan Nzyungu akisoma taarifa ya utekelezaji wa kipindi cha miaka mitano
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kwa kipindi cha miaka mitano Baraza la madiwani limeweza kufanya kazi kwa ushirikiano na Halmashauri bila kuweka itikadi za vyama vyao
Dc amesema Maendeleo hayana Chama hivyo madiwani waliweza kusimamia miradi mbalimbali ambayo imefanyika katika kata zao ili wananchi waweze kupata huduma mbalimbali za kijamii
“Niwapongeze madiwani kwa kipindi chenu cha udiwani mmeweza kushirikiana vizuri na Halmashauri na wataalamu wetu ili kuiletea maendeleo Wilaya yetu bila kujali toafuti za itikadi ya vyama nawapongeza sana,"amesema Waryuba
Wakuu wa Idara na Vitengo waliohudhuria kuvunjwa kwa baraza hilo
Aidha naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la madiwani Salum Makuyeka wakati akivunja baraza hilo amesema kuwa wanotarajia kugombea tena wafuate utaratibu na ambao hawatafanikiwa kupata wawe mabalozi wema katika maeneo yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa