Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kaya maskini7250 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zitaendelea kunufaika na mpango wa mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF baada ya kuhakikiwa huku kaya 150 zimeoondolewa kwenye mpango kwa sababu mbalimbali
Akitoa tathimini ya zoezi la uhakiki kaya maskini Mratibu wa TASAF Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi amesema kuwa idadi hiyo imepatikana baada ya walengwa waliokosa kuhakikiwa katika kipindi cha pili awamu ya tatu kilichofanyika mwezi agosti kurudiwa mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi
“Baada ya zoezi la uhakiki mwezi huu Disemba kwa kaya ambazo hazikuhakikiwa mwezi Agosti sasa katika Halmashauri yetu wanuifaika ni kaya 7250 ambao wataendelea na mpango wa malipo ,”amesema Mratibu
Mratibu amesema katika tathimini hiyo kaya 88 zimeondolewa katika mpango baada ya wakuu wa kaya kufariki dunia na hawana wanufaika,kaya 70 zimebainika kuhama makazi yao ya awali na kuhamia maeneo mengine
Wanufaika wa mpango wa TASAF
Aidha amesema katika zoezi hilo la uhakiki wa Disemba kaya 480 kati ya kaya 755 zimehakikiwa taarifa zao na matokeo yake ni kaya 480 zimehakikiwa na zitaendelea na mpango,kaya 2 zimejitoa baada ya kujitosheleza
Wanufaika wakiwa kwenye ofisi ya kijiji cha Chikongola
“Zoezi limefungwa rasmi,nawasihi walengwa endapo wataona katika taarifa zao kuna makosa yamejitokeza wasisite kutoa taarifa kwa watendaji wa vijiji na ambao watakuwa na malalamiko fomu zipo maalum kwa ajili ya kujaza,”amesema Mratibu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa