Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe Kanali Patrick Sawala amewataka wakulima kununua pembejeo katika maduka rasmi ili kuepuka kupata pembejeo ambazo zinawea kuleta madhara kwenye mikorosho
Dc Sawala akiongea na wananchi wa Kata ya Kitama
Ameyasistiza hayo kwa nyakati tofauti akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe. Katani Katani na Wakuu wa Idara kwenye ziara zake za kujitambulisha na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Miuta na Kitama ambapo amewatahadhalisha kuwa makini na wauzaji holela wa viuatilifu wanaopita katika mitaa na vijiji
Wananchi wa kata ya Kitama wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya (Hayupo pichani)
“Kuna uuzaji holela wa viuatilifu katika maeneo mbalimbali unafanywa na watu wasio waaminifu ,wakulima msinunue nendeni mkanunue kwenye maduka rasmi ambayo yanauza pembejeo endapo kuna tatizo ni rahisi kufuatilia kuliko hao wapita njia na tukiwakamata tutawachukulia hatua kali,”amesema Dc Sawala
Dc Sawala akiongea na wananchi wa kata ya Miuta
Aidha amesema pembejeo ambazo zimetolewa na serikali kwa wakulima zinaendelea kusambazwa katika vyama vya msingi (amcos) kwa usimamizi maalumu ili wakulima waweze kunufaika na pembejeo hizo
Dc Sawala (kushoto) akimsikiliza katibu wa Amcos ya Dinyanga iliyopo kata ya Kitama kuhusu ugawaji wa pembejeo katika amcos hiyo
“Sasa hivi nimeweka utaratibu maalum katika ugawaji wa pembejeo hizi,kwaiyo itagawiwa kwa wakulima kwa kufuata haki na utaratibu ili wakulima wanufaike na pembejeo hizi,na ninapita mwenyewe kwa baadhi ya amcos ili kujiridhisha endapo zoezi hili linafanyika kwa kuzingatia haki,”amesema Dc Sawala
Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wakifuatilia mkutano huo
Naye Mbunge Wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani amesema ataendelea kusimamia ili thamani ya zao la korosho ya Tandahimba iendelee kubaki kuwa juu kwasababu ndiyo wazalishaji wakubwa wa zao hilo na hawana historia ya kuwa na korosho mbovu
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe. katani akisema neno kwa wananchi wa kata ya Miuta
Katika ziara zake Dc Sawala ameendelea kuwasistiza wazazi kuhakikisha watoto wanahudhuria shule kutokomeza vitendo vya utoro na mimba mashuleni,wananchi kuendelea kuzingatia maelekezo yanayotolewa na idara ya afya kuhusu UVIKO-19,kushiriki katika miradi ya maendeleo,kuendelea kulinda amani na utulivu ndani ya wilaya sambamba na watendaji kupata taarifa za wageni wanaofika katika maeneo yao kwa kuwaoredhesha kwenye vitabu vyao vya wakazi
Wananchi wa Kata ya Miuta wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Kanali Sawala
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa