Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea siku ya Wanawake Duniani machi 8,2023 Asasi za Kiraia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba zimekabidhi vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum waliopo katika shule ya msingi Mahuta bondeni kata ya Mahuta
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika Machi 6,2023 shuleni hapo sambamba na kufanya usafi wa mazingira
Asasi zilizoshiriki ni Shirika la Wanawake wenye Uthubutu Tandahimba (WAO)TWAO,TABUFO na SDA ambapo wameahidi kuwakatia bima ya afya ya ICHF wanafunzi 29 ili waweze kupata huduma za afya
Maadhimisho ya Kilele cha siku ya mwanamke Kimkoa yatafanyika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba katika kiwanja cha Shule ya msingi Amani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa