Maafisa Waandikishaji Wasaidizi (ARO-Kata) Jimbo la Tandahimba wametakiwa kuwa na bidii,weledi ushirikiano,uadilifu na kujituma wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi.
Akufungua mafunzo hayo ya siku mbili leo Januari 21,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Afisa Mwandikshaji Jimbo la Tandahimva ndugu Aloyce Massau amewahimiza kuzingatia maelekezo ya wakufunzi ili kufanikisha utekelezaji wa jukumu hilo kwenye maeneo yao sambamba na utunzaji wa vifaa kwa usahihi na uaminifu.
Aidha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi hao wamekula kiapo cha kutunza siri na tamko la kujiondoa uanachama mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Tandahimba Mhe Joseph Waruku.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linatarajiz kuanza Januari 28 hadi Februari 3,2025 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Mwaka
2025.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa