Na Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea msimu wa Korosho Viongozi wa vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa kuzingatia ubora wa korosho wanazopokea katika maghala yao
Akifungua kikao kazi cha viongozi wa vyama vyote vya Ushirika vya msingi Oktoba 17,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Katibu Tawala Wilaya ya Tandahimba Ndg.Juvenile Mwambi amesema kuwa viongozi wa Amcos wana nafasi kubwa ya kuhakikisha Korosho inayoingia katika ghala zina ubora unaotakiwa
“Tunaelekea kwenye msimu wa 2022/2023 natoa wito kwenu viongozi wa Amcos kuhakikisha Korosho mnazopokea katika maghala yenu zina ubora unaotakiwa mjiridhishe kabla hazijapelekwa katika Ghala Kuu,”amesema Katibu Tawala
Naye Meneja wa Tanecu Tandahimba Bi.Sababu Juma amesema kuwa maandalizi ya mauzo ya Korosho kwa msimu 2022/2023 yamekamilika ambapo Mnada wa kwanza utafanyika Oktoba 21,2022 katika kijiji cha Mitondi B Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Mussa Gama alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Tanecu kwa kuwa miongoni mwa vyama bora Nchini kusimamia Korosho
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa