Na Kitengo cha Habari na Mawasilano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Sebasian Waryuba amesema wazazi , walezi na jamii kwa ujumla wana wajibu wa kuwatunza watoto na kuwapatia mahitaji muhimu sambamba na kuwalinda na vitendo vya kikatili ambavyo vinaweza kuwapata katika maeneo yao
Watoto nawazazi ambao wamehudhuria katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kijiji cha Mitondi B
Ameyasema hayo kwenye siku ya maadhimisho ya mtoto wa afrika yenye kauli mbiu ya "Tutekeleze ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za watoto" ambayo Kiwilaya yamefanyika katika kijiji cha Mitondi B kata ya Kitama, Dc Waryuba akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji,kamati ya Ulinzi naUsalama na wakuu wa idara na viteng alianza kwa kupokea maandamano ya watoto waliobeba mabango yenye jumbe mbalimbali
Dc Waryuba akisistiza umuhimu wa kuwalinda watoto katika jamii kwenye maadhimisho hayo
“Watoto hawa wana haki ya kupata elimu,afya bora,chakula,kutetewa,kuwalinda,kuwatunza ,wajibu wa mzazi na mlezi ni wa kudumu kuhakikisha mtoto anapata haki zake,wazazi mzingatie watoto wanahudhuria shule wasiwe watoro wa shule ,”amesema Dc Waryuba
Dc Waryuba (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa Mitondi B
Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg Said Msomoka akitolea majibu ya changamoto ambazo zimetolewa na mwenyekiti wa kijiji hicho ya zahanati na uhaba wa walimu amesema kuwa kwa mwaka unaokuja zahanati imetengewa Mil 40 ambazo zitakuja kufanya kazi ili watoto na jamii kwa ujumla wapate huduma stahiki
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka akitoa neno kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
“ Kwa mwaka huu wa fedha unaoanza mwezi ujao zimetengwa mil 40 lakini tutajitahidi tufanye haraka ili huduma za wagonjwa wa nje zianze mapema kwa suala la uhaba wa walimu tumelichukua,”amesema ndg Msomoka
Kamati ya Ulinzi na usalama na wakuu wa idara na vitengo ambao pia walihuduruia maadhimisho hayo
Aidha katika maadhimisho hayo Dc Waryuba alikabidhi taulo za kike kwa mratibu wa elimu kata na matroni ambazo zilitolewa a taasisi ya Search for Common Ground ambayo imetoa taulo 1000 na shirika la Sports Development Aid wametoa taulo 60 za kike na kusistiza kuwa taulo hizo ziwafikie wahusika
Maadhimisho ya mtoto wa Afrika Wilaya ya Tandahimba yamelenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa masuala ya kupinga ukatili dhidi ya watoto lengo ni kuhakikisha watoto wanakuwa salama kuanzia ngazi ya Familia kijiji,kata na Wilaya na kupambwa na burudani mbalimbali
Igizo la bunge la watoto
Wanafunzi wakiimba ngonjela kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kijiji cha Mitondi B
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa