Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Tandahimba Said Msomoka amewataka Bvr kit operator na waandikishaji wasaidizi kuifanya kazi hiyo kwa uadilifu na uamnifu ili kulinda vifaa vya Serikali ambavyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa.
Ameyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba
“Tumewaamini ndiyo maana tumewachagua tunaomba mkaifanye kazi hii kwa uadilifu na uaminifu katika vituo vyenu ,mzingatie yote ambayo mmeelekezwa na wawezeshaji katika kufanikisha zoezi hili ,”amesema Msomoka
Naye Afisa Mwandikishaji Msaidizi Ahmada Suleiman aliwaeleza kuwa ni muhimu kuzingatia muda wa kufungua na kufunga vituo kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kupata haki yako ya kujiandikisha
“Hatutarajii vituo vichelewe kufunguliwa kwakuwa kunawanachi wanahitaji kupata huduma mapema ili waweze kuendelea na shughuli zao za maendeleo lakini pia hatutakuvumilia wewe ambaye utafunga kituo kabla ya muda kwa kisingizio watu hakuna hilo halitavumilika kwakuwa muda uliopangwa uzingatiwe,”amesema Suleiman
Zoezi hili la mafunzo kwa Bvr kit na waandikishaji wasaidizi wa vituo limefanyika kwa umakini ili kuhakikisha tahadhari za ugonjwa wa corona unazingatiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa