Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka amesema abiria watakaoingia kutoka Dar es salaam na maeneo mengine nje ya Halmashauri watapimwa katika stendi kuu ya mabasi mara wanavyoingia
Ameyasema hayo jana kwenye majumuisho ya ziara fupi ya wakuu wa idara waliotembelea maeneo yaliyotengwa , zahanati ya Mtegu na kituo maalum nje ya hospital kwa ajili ya wagonjwa wa Corona Virus endapo watapatikana ndani ya Wilaya
“Kujikinga ni bora , nasi kama Halmashauri tumeamua kuchukua hatua ya kupima abiria wanaoingia kutoka Mikoa mingine ikiwa ni hatua ya mojawapo ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu kwa wananchi wa Tandahimba,”amesema Msomoka
Amesema mabasi yaendayo Dar es salaam kutoka hapa abiria watanawa mikono wanavyoingia ndani ya gari na yanayoingia pia watanawa na kupimwa joto la mwili mara baada ya kushuka ndani ya basi alilopanda
Aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid – 19 kwa kunawa maji kila mara ili kujikinga sambamba na kuepuka misongamano na kusalimiana kwa njia ya kupeana mikono
Naye Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya Silas Sembiko amesema vifaa vipo tayari, maeneo yametengwa sambamba na wataalamu wa afya ambao ni maalum kwa ajili ya kushughulia wagonjwa watakaopatikana
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa