Economic activities
1 Kilimo
Kama ilivyokwisha kuanishwa hapo juu, wilaya ina jumla ya eneo la mraba la kilomita 167,331. Kati ya hizi eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 166,535. Hata hivyo hekta129,507 tu ambazo ziko chini ya shughuli za kilimo. Mazao yanayolimwa ni pamoja korosho, muhogo, mtama, mpunga, ufuta, nazi na mengineyo. Baadhi ya mafanikio ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara kama vile uzalishajiwa korosho kutoka tani 15,282 mwaka 2005 hadi kufikia tani 47,682 mwaka 2011/2012, kuongeza uzalishaji wa karanga kutoka kutoka tani 1271 mwaka 2004/2005 hadi tani 3,129 mwaka 2011/2012. Wilaya pia imefanikiwa kuanzisha jumla ya vituo 3 vya kutolea elimu (resource centres) na kuimarisha udhibiti wa visumbufu vya mazao na mimea. Wilaya pia inatekeleza miradi mitatu (3) ya umwagiliaji katika maeneo ya ya Litehu, Lipalwe na Ng’apa. Miradi hii imeshaunda umoja wa umwagiliaji na kusajiliwa kisheria. Jumla ya wanachama katika miradi yote mitatu ni 201. Miradi inakamati za usimamizi na zina akaunti Benki.
Ubanguaji korosho katika Kiwanda cha Amama
2 Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Wilaya ina jumla ya ngombe 319 wa maziwa, mbuzi 289,975, kondoo 53,436 na wanyama wengineo. Lengo ni kuwa na miundombinu muhimu kwa ajili ya kuendeleza tasnia ya mifugo. Ili kutekeleza sheria ya nyama No. 10 ya mwaka 2006 ya kuhakikisha kuwa nyama inayoliwa ni salama. Halmashauri kupitia idara ya Mifugo na Uvuvi imejenga machinjio 2, malambo 3 kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo yamejengwa na kujenga kliniki mojakwa ajili kutambua kimaabara magonjwa ya mifugo. Kwa upande wa uvuvi, idara imefanikiwa kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki kwa wafugaji binafsi nakushauri wafugaji kuchimba mabwa wa kwa ajili ya kufuga samaki. Baadhi ya changamoto zinazoikabili wilaya katika mifugo ni pamoja na upungufu wa maafisa ugani ambao idadi yao haitoshi kusimamia shughuli za kilimo na mifugo na uvuvi katika wilaya, ufinyu wa bajeti ili kununua chanjo na mafuta ili kuwafikia wafugaji wengi zaidi pamoja na bei kubwa ya chanjo. Kwa hiyo Wilaya inakusudia kuimarisha huduma za ugani kwa wafugaji. Hii ni pamoja na kuongezeka kwa uzito wa ng’ombe kutoka kilo 250 hadi 350, kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa ng’ombe kwa mwaka kutoka lita 400 hadi 2000, na kuongezeka kwa mbuzi walioboreshwa kutoka 217 – 3800 ifikapo 2018ifikapo mwaka 2018. Wilaya pia inalenga kuongeza idadi ya vijiji vilivyotenga maeneo ya malisho na kuanzishwa kwa vikundi vya wafugaji vitano (5) vinavyotumia nishati ya gesi (Bio-gas) ya kupikia ifikapo 2018
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa