HALMASHAURI YA WILAYA YA TANDAHIMBA
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA KWANZA (JULAI - SEPTEMBA) 2017
Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeidhinishiwa kupokea na kutumia jumla ya shilingi 7,770,772,000.00 Katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Dira ya Maendeleo Ya Taifa ya mwaka 2025 (Vision 2025), Sera mbalimbali za Kisekta pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Hii ni kutokana na Dira na Dhima ya Halmashauri kwamba “ Ifikapo 2018 Halmashauri Ya Wilaya Ya Tandahimba, Kwa Kutumia Rasilimali Zilizopo, Utalaamu Na Ushirikishwaji Wa Jamii, Iwe Imetoa Huduma Bora Na Kujenga Uchumi Endelevu Utakaowezesha Maisha Bora Ya Wananchi’’
Fedha hizo zilitarajiwa kuchangiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Mapato ya ndani ya Halmashauri (OwnSource), Ruzuku ya Maendeleo toka Serikali Kuu (LGCDG), Ruzuku ya Kujenga Uwezo (CBG), Mfuko wa Barabara (Road Fund), Mfuko Kamambe wa Afya (Health Sector Basket Fund), Mfuko wa Maji (RWSSP), United Nations International Children's Emergency Fund (UNICEF), Mfuko wa Jimbo, pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Mchanganuo wa fedha hizo kwa wachangiaji walioainishwa hapo juu kwa mwaka 2017/2018 ni kama unavyoonekana kwenye jedwali:-
NA
|
CHANZO/MCHANGIAJI |
MAKISIO |
FEDHA TOLEWA |
FEDHA TUMIKA |
FEDHA ZISIZOPOKELEWA |
% YA FEDHA TOLEWA |
1 |
OWNSOURCE
|
3,925,627,000.00
|
152,977,720.0
|
152,977,720.0
|
3,772,649,280.0
|
3.90
|
2 |
LGCDG
|
1,329,173,000.00
|
|
|
1,329,173,000.0
|
-
|
3 |
MFUKO WA MAJI
|
2,375,725,000.00
|
|
|
2,375,725,000.0
|
-
|
4 |
MFUKO WA JIMBO
|
51,909,000.00
|
25,954,500.0
|
|
25,954,500.0
|
50.00
|
5 |
UNICEF
|
88,338,000.00
|
101,711,150.0
|
75,537,000.0
|
(13,373,150.0)
|
2.59
|
6 |
TASAF
|
|
1,100,120,080.0
|
1,098,563,080.0
|
|
|
|
JUMLA
|
7,770,772,000.00
|
1,380,763,450.0
|
1,327,077,800.0
|
7,490,128,630.0
|
35.17
|
Hadi kufikia tarehe 30/09/2017 tulipomaliza robo ya kwanza, Halmashauri ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 1,380,763,450.0 na kutumia jumla ya Shilingi 1,327,077,800.0 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo sawa na asilimia 35.17 ya fedha yote iliyoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2017/2018.
Aidha kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF katika robo ya kwanza halmashauri ilipokea jumla ya Shilingi 216,910,880.00 kwa ajili ya ruzuku ya walengwa wa kaya maskini na kutumia jumla Shilingi 186,816,000.00 kwa ajili ya malipo kwa kaya maskini. Hata hivyo Shilingi 212,000.00 zimerejeshwa TASAF Makao Makuu kutokana na baadhi ya walengwa kukosa sifa za kulipwa fedha hizo ikiwa ni pamoja na vifo au kuhama makazi. Pia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia TASAF jumla ya shilingi 883,209,200.00 zimepokelewa na kiasi cha shilingi 881,863,600.00 kimetumika katika utekelezaji wa miradi na ujira kwa walengwa wanaoshiriki utekelezaji wa miradi
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri imepokea jumla ya shilingi 101,711,150.0 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa UNICEF kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa usajili na utoaji wa yeti vya kuzaliwa kwa watoto kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) bila malipo.
Mchanganuo wa miradi hiyo na utekelezaji wake kifedha na kimaumbile umeonyeshwa kwenye majedwali yaliyombatanishwa kuanzia ukurasa wa 1 hadi 12 kwa miradi ya mwaka 2017/2018 na miradi viporo ya mwaka 2017/2018 iko katika ukurasa wa 13
Abdillah L Mfinanga
Kny: Mkurugenzi Mtendaji (W)
TANDAHIMBA
Mchanganuo wa miradi ni kama unavyoonekana kwenye kiambatisho hapo chini
MIRADI ILIYOPITA MWAKA 2017.18.xlsx
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimba.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa