Huduma za Afya
Wilaya ya Tanndahimba ina jumla ya vituo 34 vya kutolea huduma za afya. Hii ni pamoja na Hospitali moja inayomilikiwa na serikali, vituo vya afya 3 kimoja kati ya vituo hivyo kinamilikiwa na shirika la Kanisa la Katoliki na vituo vingine 2 vinamilikiwa na serikali.Pia kuna zahanati 30, zahanati 29 kati ya hizo zinamilikiwa na serikali na moja inamilikiwa na mtu binafsi. Pia kuna maduka ya dawa baridi 27.
HUDUMA ZA UCHUNGUZI
Katika kuendeleza na kufuata kanuni za utoaji wa huduma bora za afya , hospitali imekuwa ikitoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kabla ya mgonjwa kuanzishiwa matibabu. Huduma hizo za uchunguzi zinafanywa kupitia maabara iliyopo ambayo ina uwezo wa kufanya uchunguzi wa takribani vipimo vyote vya msingi , kwa kipindi cha mwezi January-December 2016 vipimo mbalimbali vilifanyika kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo chini
KIPIMO
|
Extremities
|
Chest x-ray
|
Pelvis
|
Skull
|
Cervical Spine
|
Lumber Spine
|
Thoracic/Spine
|
Lumber Sacral
|
Abdominal X – ray
|
Barium Swallow
|
Barium meal
|
Obstretic ultrasound
|
Intravenous Urography
|
Hystero Salpingograph
|
HUDUMA ZA DAMU SALAMA
Hospitali inatoa huduma za upasuaji hata hivyo katika kuboresha huduma za dharura kwa wagonjwa wanaohitaji damu wakati wa upasuaji pamoja na wagonjwa wenye upungufu wa damu, hospitali inaendesha zoezi la ukusanyaji damu na kuanzia mwezi may 2016 jumla ya sampuli 846 za damu zilikusanywa. Kati ya hizo units 751 zimetumika.
Zoezi la ukusanyaji damu linakabiliwa na changamoto za mara kwa mara za upatikanaji wa mifuko ya kuhifadhia damu pia mwamko mdogo katika uchangiaji toka kwenye jamii
Huduma za uzazi na watoto
Katika kuboresha huduma kwa wajawazito halmashauri imekuwa ikiendelea kutoa huduma za chanjo, upimaji wa wingi wa damu pamoja na kutoa elimu kwa wajawazito juu ya utambuzi wa dalili hatari kwa mjamzito pamoja na kusisitiza wajawazito kuwahi kliniki na kujifungulia katika vituo vya huduma za afya. Aidha halmashauri imeendelea kufutailia uwepo wa dawa muhimu kwa wajawazito wakati wa kujifungua ikiwemo dawa za Oxtocin na Magnesium Sulphate. Pia halmashauri inatoa huduma za upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito katika vituo vya afya viwili na hospitali moja.
Mapambano dhidi ya ukimwi
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ni kipaumbele kimojawapo halmashauri ina jumla ya vituo 33 vinavyotoa dawa za kufubaza VVU kwa wananchi wanaoishi na VVU. Aidha katika maambukizi mapya Halmashauri imekuwa ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kujikinga na maambukizi ya VVU. Hata hivyo kwa upande wa watumishi imekuwa ikihakikisha kuwepo kwa vifaa vya kusaidia kuwakinga watumishi wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa. Aidha halmashauri bado imekuwa ikiendelea kuendesha vikao na kutoa elimu kwa vikundi vya kina mama wajawazito wanaoishi na VVU kwa lengo la kuwakinga watoto wasizaliwe na VVU. Pia halmashauri kwa kupitia vituo vyake 12 vya huduma za afya vimekuwa ikiendelea kutoa huduma ya kupima kinga za mwili (CD-4) kwa wananchi wanaoishi na VVU kila baada ya miezi sita pamoja na kuchukua damu za watoto waliozaliwa na kina mama wenye VVU kwa ajili ya upimaji wa VVU. Hadi sasa jumla ya wanaoishi na virusi vya ukimwi ni 5,081 kati yao wanaume ni 1,655 na wanawake ni 3,426.Mammbukizi ya ukimwi kwa sasa ni 3% katika wilaya.
HUDUMA ZA MAABARA.
VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA:
Halmashauri ina jumla ya vituo 4 vya kutolea huduma za maabara katika vituo hivyo Hospitali 1inayomilikiwa na Serikali.Vituo vya Afya 3 kimoja kati ya hivyo kinamilikiwa na shirika la Dini.Vituo vingine 2 vinamilikiwa na Serikali.
JINA LA KITUO
|
AINA KITUO
|
MMILIKI
|
TANDAHIMBA HOSPITALI
|
HOSPITALI
|
SERIKALI
|
NAMIKUPA
|
KITUO CHA AFYA
|
SERIKALI
|
MAHUTA
|
KITUO CHA AFYA
|
SERIKALI
|
LUAGALA
|
KITUO CHA AFYA
|
SHIRIKA LA DINI
|
HUDUMA ZA MAABARA ZINAZOTOLEWA HOSPITALI YA WILAYA
>Upimaji wa kinga mwili (CD4 Testing)
>Upimaji wa Vikope vya VVU kwenye Damu (Viral Load)
>Huduma ya Daamu Salama (Blood Transfusion)
>Upimaji wa makundi ya damu na Compatibility Test.
>Upimaji wa uwingi wa Damu (HB)
>Upimaji wa MALARIA.
>Upimaji wa Sukari kwenye Damu
>Upimaji wa Kaswende kwenye Damu
>Upimaji wa CHOO haja Kubwa
>Upimaji wa MKOJO
>Upimaji wa makohozi (TB).
>Upimaji wa PITC
>FBP
>S.CREATININE na ALAT/ASAT
HUDUMA YA DAMU SALAMA.
Banki ya Damu ya Hospitali ya Wilaya inapata Damu kwa njia Uchangiaji damu wa hiari.
MAENEO YA UCHNGIAJI DAMU:
>Shule za Sekondari.
>Taasisi za Dini (Kanisani& Misikitini) na
>Viwandani.
Sampuli za Damu hupelekwa Banki ya Damu ya Kanda ya Kusini (SZBTS) MTWARA.
Sampuli za Damu huchunguzwa magonjwaa makubwa manne.(Four Markers)
>HIV
>HBV
>HCV na
>KASWENDE (Syphilis)
Mwaka 2016 Jumla ya chupa 846 za Damu zilikusanywa.
Sampuli 95 Zilionekana kuwa na maambukizi mbalimbali:
>HIV sampuli 27= (3.19%)
>HBV Sampuli 35= (4,1%)
>HCV Sampuli 8=(0.9%)
>SYPHILIS Sampuli 25 =(2,9%)
VIPIMO VYA MALARI 2016:
Jumla ya Vipimo vyote vya malaria
|
42039
|
Positive Malaria
|
16701
|
VIPIMO VYA WEKUNDU WA DAMU:
Jumla ya vipimo vyote vya HB
|
7116
|
HB chini ya 70g/L(5O%)
|
925
|
VIPIMO VYA KASWENDE:
Jumla ya vipimo vyoyte vya kaswende
|
1945
|
Positve Syphilis
|
152
|
VIPIMO VYA SUKARI KWENYE DAMU:
Jumla ya vipimo vyote vya sukari
|
3199
|
Juu ya 10mmol/L(180mg/L)
|
589
|
VIPIMO VYA CHOO( HAJA KUBWA)
Jumla ya vipimo vyote vya choo
|
1655
|
Positive H/Worms
|
41
|
VIPIMO VYA MKOJO:
Jumla ya vipimo vyote vya mkojo
|
8025
|
Posittive S.Haematobium
|
32
|
VIPIMO VYA MAKOHOZI:
Jumla ya vipimo vyote vya makohozi
|
1416
|
Positive AFB
|
156
|
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimba.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa