IDARA NA VITENGO
1. MIPANGO,TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Majukumu ya Idara ya Mipango na Ufuatiliaji ni kama ifuatavyo:-
2.ELIMU YA MSINGI
MAJUKUMU YA IDARA ELIMU MSINGI
1.Kuratibu mitihani ya ndani na nje ya wilaya
2.Kufanya tathimini ya mitihani mbalimbali
3.Kusimamia usajili wa wanafunzi
4.Kuratibu elimu msingi, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi
5.Kuthibiti takwimu za wanafunzi,walimu,majengo na samani
6.Kusimamia taaluma katika wilaya
7.Kufanya tafiti mbalimbali za kielimu
8.Kusimamia uboreshaji wa mazingira ya shule
9.Kusimamia elimu ya kujitegemea na lishe shuleni
10.Kusimamia miradi ya maendeleo iliyoelekezwa shuleni
11.Kusimamia matumizi ya fedha za ruzuku za uendeshaji shuleni
12.Kuendesha mafunzo mbalimbali ya kuinua taaluma za walimu
13.Kuratibu elimu kwa wanafunzi wenye maalumu
14.Kuratibu na kusimamia vituo vya ufundi stadi
15. Kusimamia na kuratibu michezo na sanaa za maonesho
3 IDARA YA ELIMU SEKONDARI
KAZI KUU ZA IDARA HII.
Kuratibu shughuli zote za matumizi ya fedha za Elimumsingi msingi bila malipo katika shule
Kukusanya, kuchambua na kuwasilisha takwimu muhimu za idara kadiri zinapohitajika.
Kusimamaia utawala bora mashuleni.
Kuandaa taarifa za robo mwaka za utekelezaji wa maendeleo ua elimu na kuwasilisha WEMU na OR- TAMISEMI
Kutoa mapendekezo ya uteuzi wa wakuu wa shule
Kushughulikia uhamisho wa walimu na watumishi wasio walimu na wanafunzi ndani ya Halmashauri
Kutathmini utendaji kazi wa walimu na watumishi wasio walimu
Kusimamia utekelezaji wa taarifa ya ukaguzi wa shule
Kuratibu utekelezaji wa taarifa ya ukaguzi wa shule
Kuratibu na kuendesha vikao vya idara
4.IDARA YA AFYA
1.0 UTANGULIZI:
Idara ya Afya, imegawanyika katika Vitengo vikuu viwili, ambavyo ni kitengo cha Afya Tiba na Afya Kinga. Aidha idara hii inahudumia wananchi kupitia jumla ya Vituo 36 vya kutolea huduma za Afya.vikiwemo vya Serikali 33, watu Binafsi 3 kama inavyoonekana katika Jedwali hapa chini:-
KITUO CHA HUDUMA
|
SERIKALI
|
BINAFSI
|
MASHIRIKA
|
JUMLA
|
Hospitali ya Wiaya
|
1
|
0
|
0
|
1
|
Vituo vya Afya
|
3
|
0
|
0
|
3
|
Zahanati
|
29
|
3
|
0
|
32
|
Jumla:
|
33
|
3
|
0
|
36
|
MAJUKUMU YA IDARA YA AFYA
5.MAENDELEO YA JAMII, USTAWI WA JAMII NA VIJANA
1.0 UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii inahusika zaidi na kuraghibisha jamii ili iweze kushiriki kikamilifu katika Maendeleo,hii ni pamoja na kubadilisha,mitazamo,fikra,tabia,na mienendo ili iwe chanya kwaajili ya Maendeleo ya wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Kuiwezesha jamii kuibua kupanga na kutekeleza kwa kikamili yale waliyopanga kwa kutumia zaidi raslimali zilizopo maeneo yao na za nje pale zitakapohitajika
Idara ina madawati matano na Kitengo kimoja (1) kama ifuatavyo :
1.MADAWATI:
2.Utafiti na Mipango
3.Dawati la Jinsia na Watoto
4.Kikosi cha Ufundi na Ujenzi
5.Uwezeshaji wananchi kiuchumi
2.VITENGO
1.Idara ina Kitengo kimoja cha vijana
3.0 Pia Idara ina ratibu shughuli zifuatazo
1.Uratibu wa VICOBA
2.Uratibu wa shughuli wa TASAF
3.Uratibu wa Asasi
4.Uratibu wa Shughuli za Mwitiko wa Jamii katika kudhibiti UKIMWI
4.0 MAJUKUMU YA IDARA :
1.Kuhamasisha na kuiwezesha jamii,kushiriki katika kutambua, kuibua, kupanga , kutekeleza, kufuatilia na kutathimini shughuli zao za Maendeleo.(To ensure that community Participate fully in formulating, Planning, implementing and evaluating Development Plans.
2.Kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli zote za Maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi ya kijamii,usafi wa mazingira
3.Kusimamia na kuhamasisha shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake ,vijana , vikundi vingine vya kiraia
4.Kuratibu shughuli za Mwitiko wa jamii katika kudhibiti UKIMWI
5.Kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora na uimarishaji wa vikosi vya ujenzi vya Kata vikiwemo vya vijana
6.Kuhamasisha shughuli zote za Maendeleo ya watoto .
7.Kukusanya takwimu mbalimbali za Maendeleo ya Jamii kwaajili ya Mipango ya Maendeleo ya jamii
8.Kuwezesha wanawake na vijana kuongeza kipato chao kupitia fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo, utoaji wa mikopo kwa vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake na vijana kupitia mfuko wa Maendeleo wa Wanawake na vijana wa Halmashauri
9.Kuratibu shughuli zote za Asasi
10.Kuziwezesha jamii kutambua fursa walizonazo ili kutatua vikwazo vya maendeleo (mipango shirikishi).
11.Kujenga uwezo wa Halmashauri na vijiji juu ya utawala bora, upangaji mipango shirikishi na bajeti.
12.Kueleimisha jamii kuingiza masuala mtambuka katika mipango,bajeti, na shughuli za maendeleo kama usafi wa mazingira, mapambano dhidi ya UKIMWI, Mapambano dhidi ya rushwa na Jinsia
6. KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
MAJUKUMU YA IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
1.Kutoa ushauri wa kilimo bora katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
2.Kusimamia shughuli za kilimo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
3.Kuunganisha wakulima na wadau mbalimbali ndani na nje ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
4.Kuunganisha wakulima na masoko ndani na nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
5.Kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
6.Kutoa elimu ya uendeshaji wa vyama vya ushirika ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
7.Kukagua vyama vya ushirika na kutoa ushauri ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
8.Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba
9.Kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
10.Kutoa taarifa za tahadhari mfano ukame, mafuriko, uwepo wa magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu na jinsi ya kukabiliana.
11.Kusimamia na kuhakikisha kuwa miradi ya kilimo inatekelezwa
12.Kuandaa taarifa na kuwasilisha katika mamlaka husika
13.Kuandaa mpango na bajeti ya idara ya Kilimo
14.Kuunganisha wakulima na makampuni yanayouza zana za kilimo
7. MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI
Idara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi inasimamia shughuli zote za ufugaji na uvuvi katika halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
MAJUKUMU YA IDARA
8. IDARA YA ARDHI
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SEKTA YA ARDHI
Umilikishaji Ardhi Mjini
Katika mwaka 2016/17 sehemu ya ardhi imeweza kutayarisha hati za kawaida zipatazo 134, inayofanya jumla ya hati kuwa 383.
Umilikishaji Ardhi Vijijini
Kwa mwaka 2016/17 idara imeweza kuandaa hati 22 kufanya jumla ya hati zote kuwa 4734 za mashamba vilevile utaratibu wauandaaji wa hati za kimila kwa maeneo ya umma na majengo ya serikali yaliyopo vijijini unaendelea.
Mipango Miji na Upimaji Ramani.
Kwa mwaka 2016/17 idara imeanza kupima eneo la Shule ya msingi Amani na barabara ya mivanga ambapo tunategemea kupima viwanja 200 ambavyo vitauzwa na Halmashauri.
Mchoro wa mipango miji wa kwanza uliandaliwa mwaka 1979 na mpaka sasa tuna michoro ya mipango miji 14 na michoro kumi iko katika matayarisho.
Jedwali na. 1.1: Michoro ya mipango miji Tandahimba
Na. |
Namba ya Mchoro |
JIna |
Idadi ya viwanja |
Viwanja vilivyopimwa |
Maelezo |
1
|
52/MT/2/1290
|
Tandahimba Secondary School
|
2 |
2 |
Upimaji unaendelea
|
2
|
45/7/298
|
Tandahimba Central area
|
1030 |
1030 |
Upimaji umekamilika
|
3
|
45/9/299
|
Mji Mpya
|
308 |
110 |
Upimaji umekamilika
|
4
|
45//TAND/01/600
|
Central area amendment
|
176 |
105 |
Upimaji umekamilika
|
5
|
45/TAND/02/402
|
Mji Mpya – II
|
406 |
55 |
Upimaji umekamilika
|
6
|
45/TAND/03/42002
|
Mivanga Road Low Density Plots
|
545 |
11 |
Upimaji umekamilika
|
7
|
45/TAND/04/112003
|
Hospital Plot Expansion
|
129 |
129 |
Upimaji umekamilika
|
8
|
45/TAND/05/112004
|
Majengo
|
88 |
18 |
Upimaji umekamilika
|
9
|
45/TAND/06/112004
|
Petrol Station Plot
|
13 |
13 |
Upimaji umekamilika
|
10
|
45/07/179A
|
Amendment of TP Drawing No. 45/07/179
|
33 |
33 |
Upimaji umekamilika
|
11
|
03/TAND/14/032015
|
Proposed Mivanga Road Layout Plan
|
335 |
16 |
Upimaji umekamilika
|
12
|
03/TAND/15/032015
|
Proposed Matogoro Neighborhood Unit Layout
|
548 |
45 |
Upimaji unaendelea
|
13
|
03/TAND/16/032014
|
ProposedSquatter Upgrading At Old Tandahimba – I
|
247 |
10 |
Upimaji unaendelea
|
14
|
03/TAND/17/032014
|
Proposed Mji Mpya Squatter Upgrading - I
|
419 |
08 |
Upimaji unaendelea
|
Vilevile katika kipindi hiki idara imeanza utaratibu wakuhuisha baadhi ya vijiji na kuwa maeneo ya mpango (Planning Areas) takribani vijiji 44 kutoka kata zote vimependekezwa kuwa maeneo ya mipango ambapo mipango ya kina inaendelea kuandaliwa kadri muda unavyozidi kuendelea na kutokana na mahitaji ya eneo husika. Hii ni kutokana na maagizo ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI) ya kusimamia miji midogo inayoibukia ilikudhibiti uendelezaji holela wa makazi.
Fidia ya Ardhi na Mimea.
Kwa mwaka 2016/17 idara imelipa fidia za mimea ardhi na usumbufu kwa wananchi takribani 32 ambao wamelipwa kiasi cha Tsh.103,000,000/=, fidia hii inajumuisha eneo la Dampo Mivanga na eneo la Makaburi ya MjiMpya pamoja na maeneo mengine yaliyotwaliwa na Halamashauri tangu mwaka 2011 mpaka 2014.
9. UTUMISHI NA UTAWALA
Idara ya Utawala na Utumishi inashughulikia masuala yote yanayohusu Uendeshaji, Watumishi na Utumishi kama ifuatavyo.
Kuratibu na kushughulikia malalamiko na mashitaka.
10. IDARA YA MAJI
1.Huduma mbalimbali zinazotolewa na Idara ya Maji ni:-
2.5 Chapisho la Sheria na Taratibu za usanifu mradi (MOWI designing Manual 2007)
2.6 Zabuni zinazoendelea kutekelezwa Idara ya Maji Mwaka 2016/2017
2.11 Kazi muhimu/Nyeti za Uhai wa Idara
Miradi
4.1 Miradi iliyotengewa fedha 2016/2017
4.2 Miradi inayotekelezwa
Jina la Mrdi
|
Kazi zilizopangwa kufanywa
|
Jina la Mkandarasi anayetekeleza
|
Ghrama za mkataba
|
|
Mradi wa maji Jangwani, Maheha, Umoja, Mundamkulu na Chipyai
|
|
Eker Co.Ltd
|
|
|
mradi wa maji katika vijiji vya Litehu, Libobe, Liponde na Mkolachini
|
|
Hecle Co.Ltd
|
|
|
Mradi wa Maji Mkupete
|
|
Reni Internation Co.Ltd
|
|
|
Mradi wa Maji Mahuta
|
|
Matrix Technology Co.Ltd
|
|
|
11.FEDHA NA BIASHARA
UTANGULIZI
Idara ya fedha ni miongoni mwa idara zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, idara inatelekeza majukumu yafuatayo katika utendaji kazi katika wilaya ya Tandahimba.
12.IDARA YA UJENZI
Majukumu ya Idara ya Ujenzi
Kitengo cha Majengo
Kitengo cha Magari na mitambo
VITENGO
1.Kitengo cha Ufugaji Nyuki
2.Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
3.Kitengo cha Sheria
4.Kitengo cha Ugavi na manunuzi
5.Kitengo cha Uchaguzi
6.Kitengo cha Teknolojia, habari, mawasiliano na uhusiano
Kazi za kitengo
1. Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja naUmma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.
2 Kupokea nakushughulikia malalamiko pamoja na kuratibu masuala ya kiitifaki ikiwemokupokea wageni.
3. Usimamizi Wa Mifumo Ya Kompyuta(System Administration)eneo hili linashughulikia usimamizi na uendeshaji wa mifumo yote ya kompyutakatika Halmashauri
5. Usimamizi Wa Mtandao Wa Kompyuta Pamoja Na Vifaa Vyake(Network And Hardware Adminstration).
6. Usimamizi Wa Benki Ya Takwimu(Database Administration)
7. Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
8.Kutoa msaada wa kitaalamu kwa watumiaji wa mifumo ya kompyuta
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimba.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa