Taasisi isiyo ya Kiserikali ya GRCF (The Global Religion for Children Foundation Tanzania) na CEFA zinazotekeleza mradi wa Kujenga Amani wamekita kambi ya Siku 14 Wilaya ya Tandahimba na kutoa Elimu kwa jamii kupitia Warsha mbalimbali, kukutana na Viongozi wa Dini, Mabonanza ya michezo pamoja na kutoa Elimu Shuleni katika kata 5 za Wilaya hiyo .
Mkurugenzi wa Shirika la GRCF Joyce Mdachi amesema mradi unatekelezwa katika Wilaya tatu za Mkoa wa Mtwara ikiwemo Tandahimba ambapo wanatarajia kutoa Elimu ya ukatili wa kijinsia na namna ya kudumisha amani kwa jamii ili kujenga Jamii yenye Maendeleo endelevu.
Kwa Upande wake Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilaya ya Tandahimba Rajab Carlos amesema kupitia bonanza la Michezo na maonesho ya kuigiza yenye ujumbe wa kudumisha amani yamesaidia Wananchi hasa vijana kujiamini , kupata uelewa juu ya umuhimu wa uwepo na amani pamoja na kupinga ukatili unaoweza kusababisha uvunjifu wa Amani.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa