Shirika lisilo la Kiserikali la Road To Success Organization (ROTOSO) limefanya Kikao cha kujadili tathmini ya utendaji kazi wa Shirika hilo kupitia mradi wa " Kwa pamoja tudumishe amani" ambao umelenga kutoa Elimu kwa vikundi vya wanawake kuhusu kutatua Migogoro kwa njia ya amani .
Katika Kikao hicho mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti amehudhuria na kuwapongeza kwa kufanikiwa kutoa uelewa kwa Wananchi hasa makundi ya wanawake katika kata za Tandahimba, Nyanyanga na Nambahu ambako mradi huo inatekelezwa akiwasisitiza kuendelea katika Maeneo Mengine.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Sudi Hashimu amesema wanatarajia kuongeza wigo wa utendaji kazi wa mradi huo wa kwa pamoja tudumishe amani katika Maeneo Mengine ya Wilaya ya Tandahimba .
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa