• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

TASAF kuvifikia vijiji 69 viliyosalia Halmashauri ya Tandahimba

Posted on: April 27th, 2021

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wametakiwa  kutoa ushirikiano kwa wawezeshaji ili waweze  kupata taarifa sahihi ambazo zitawasaidia kwenye zoezi la mpango wa kunusuru kaya maskini wa  TASAF awamu ya pili kipindi cha tatu ambapo vijiji 69 vitafikiwa katika mpango huo

Akizungumza kwenye mkutano wa kijiji cha Malopokelo Afisa Ufuatiliaji wa TASAF makao makuu Bi  Judith Woiso amesema kuwa lengo la serikali ni kuwafikia wananchi  wa Kitanzania  ambao wanaishi katika hali duni  hivyo  vikao vinasaidia kuleta uwazi kwa wananchi kuwadhibitisha kwenye ngazi ya kijiji

Afisa  ufuatiliaji TASAF makao makuu bi Judith Woiso(aliyesimama) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malopokelo

“Wananchi mnatakiwa muhudhurie kwa wingi   vikao kama hivi vinasaidia kuwatambua ambao watachukuliwa taarifa zao ili  mjiridhishe kwa uwazi kuwa wanastahili kuingia kwenye mpango,pia  mpango  huu unakuja na miradi mbalimbali ambayo itawanufaisha wananchi wote wa kijiji husika si walengwa  peke yao,”amesema bi Woiso

Wananchi wa kijiji cha Malopokelo wakiwa kwenye mkutano wa kijiji  na wawezeshaji  wa TASAF

Wananchi wa  vijiji ambavyo vimefikiwa na mpango huu wa kipindi cha pili wameishukuru serikali kwa mpango huo  ambao wanatarajia utawanufaisha na kuwaondoa katika umaskini

“Tunaishukuru serikali kwa mpango wa TASAF katika vijiji  vyetu ambavyo havikufikiwa tunaamini kwa wale ambao wamekidhi vigezo mpango huu utakwenda kuwasaidia  na kuwawezesha kuishi maisha ya mtanzania wa kawaida angalau yakupata mlo wa siku,”amesema Kassim Mussa Mkazi wa Malopokelo

Mkazi wa Kijiji cha Malopokelo ndugu Kassim Mussa akitoa pongezi kwa serikali kwa kuleta mpango wa TASAF kijijini hapo

Mpango wa kunusuru kaya maskini kipindi cha pili awamu ya tatu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ulizinduliwa na Mkuu waWilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba  ambapo vijiji 69  sawa na asilimia 44 vitafikiwa ,awali mpango huu ulifikia vijiji 88 sawa na asilimia 56

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba (kati) akiwa pamoja na wawezeshaji  ngazi ya Wilaya (waliosimama),aliyekaa wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Baisa Baisa,Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi TASAF Makao makuu ndg Shedrack Mziray ,Katibu Tawala Juvenile Mwambi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri a Tandahimba Hadija Mwinuka

Wawezesha ngazi ya Wilaya  baada ya kumaliza mafunzo wameanza kufanya utambuzi katika maeneo husika  ngazi za vijiji,zoezi linaloendelea ni uchukuaji wa taarifa za kaya ambapo hadi kufikia  Mei 6, mwaka huu  zoezi hilo litakuwa limekamilika kwa vijiji 69 vilivyobaki ndani ya Halmashauri 

Mwezeshaji wa TASAF Makao Makuu ndg Joseph Elieza akitoa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa