• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

Rc Gaguti akagua maendeleo ya miradi ya vyumba vya madarasa

Posted on: December 11th, 2021

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Brig.Jen. Marco Gaguti amesema ameridhika na ubora wa kazi inayofanyika ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

Ameyasema hayo jana Desema 10,2021kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya vyumba vya madarasa Wilayani Tandahimba na kushauri kuwa katika miradi mingine yote inayoendelea kujifunza kupitia miradi hii ya Uviko -19

“Kwenye ziara hii ambayo nimefanya katika Mkoa wa Mtwara nimeridhika na maendeleo ya miradi inayoendelea katika Wilaya zote ikiwemo hii Tandahimba,lakini lipo jambo la kujifunza katika miradi hii  tujitathimini  na tujipange kuikamilisha miradi yote ambayo fedha yake ipo iweze kukamilika kwa wakati kabla ya mwaka wa fedha haujakwisha,”amesema Rc Gaguti

Aidha amesema sambamba na miradi hiyo ya elimu kuna  mdondoko wa wananfunzi  na ufaulu  ambavyo vimekuwa ni changamoto na kuwataka wazazi,walezi na madiwani  kuhakikisha wanasimamia  suala la elimu katika maeneo yao na kuhakikisha wananfunzi wanapata chakula shuleni

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali  Patrick Sawala amesema kuwa  miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa viongozi ngazi ya Halmshaauri,madiwani,viongozi wa chama cha Mapinduzi na kamati,wakuu wa shule,watendaji na wananchi kila mmoja kwa nafasi yake ameweza kushiriki katika miradi hii

“Miradi yetu ipo katika hatua ya ukamilishaji  hadi kufikia tarehe Desemba 13 tunatarajia kukukabidhi miradi hii ya vyumba vya madarasa 88 na ofisi 41 za walimu,”amesema Dc Sawala 

Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama amesema baada ya kupokea fedha kutoka Serikali kuu za ujenzi wa vyumba vya madarasa  88 ambayo gharama yake ni shilingi Bilioni 1.76 Halmashauri imeweza kujiongeza  kujenga ofisi 41 katika kila mradi

“Baada ya kupokea fedha hizi tulijiongeza kwa kila mradi wa vyumba vya madarasa tumejenga na ofisi za Walimu ili waweze kukaa katika mazingira bora,”amesema Mkurugenzi

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa