• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

RC Byakanwa aipongeza Halmashauri ya Tandahimba kupata hati safi ya CAG

Posted on: June 3rd, 2020

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ameipongeza Halmashauri ya Tandahimba kwakupata hati  safi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2018/2019

Ameyasema hayo leo kwenye kikao maalum cha Baraza la  Madiwani la kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi kuu wa hesabu za serikali(CAG) ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba


RC Gelasius Byakanwa(Kulia) akiwa na Dc Sebastian Waryuba (kushoto) kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani

“Naipongeza  Halmashauri ya Tandahimba kwa kupata Hati safi  kwa mara nyingine tena,kiongozi wa Mkoa unapata usingizi ikiwa  Halmashauri zako zinapata hati safi, nazitaka Halmashauri zote kupata hati safi ifike mahali hati chafu abaki naye yeye CAG ili sisi ijulikane kuwa ni waelewa na tunafuata utaratibu,”amesema Byakanwa 


Kamati ya ulinzi na Usalama,Wakuu wa Idara na Vitengo ambao walihudhuria baraza hilo

Aidha amesema   wataalamu wahakikishe wanakusanya mapato  kwakuwa ndiyo uti wa mgongo wa Halmashauri kwa mwaka 2018/2019 ilikadiriwa kukusanywa Bilioni 5 lakini makusanyo yaliyopatikana  ni shilingi Bilioni 1  hivyo jitihada zifanywe ili kuhakikisha mapato yanaongeza

“Hatuwezi kuendelea kuwachekea watu wanaokaa na fedha za mapato mifukoni badala ya kuja kwenye Halmashauri ili fedha hizo zirudi kwenye miradi ya maendeleo kwa wananchi,miradi mikubwa mnayoiona ni usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ,”amesema Byakanwa  



Madiwani wa Halmashauri ya Tandahimba wakiwa kwenye kikao maalum cha kujadili taarifa ya CAG


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Namkulya Namkulya amesema kuwa ndani ya miaka minne mfululuzo Halmashauri ya Tandahimba imepata hati safi  hiyo ni kudhihirisha taratibu na kanuni za fedha zinafuatwa



Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri  ya Tandahimba Namkulya Namkulya (kulia) akielezea jambo (kushoto) Rc Byakanwa

“Hii ni mara  ya nne kupata hati safi mfululizo kwa Halamsahuri yetu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuanzia tumeingia madarakani sisi madiwani,tunafarijika kwa jambo hili,”amesema Namkulya 

 

 

 





Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa