JANUARI 17,2025
Maafisa ugani Kilimo walioajiriwa na Bodi ya Korosho Tanzania wametakiwa kuwa na bidii na Uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kufikia malengo ya Serikali ya uzalishaji wa Korosho Tani 700,000 msimu wa mwaka 2025/2026 .
Akifunga mafunzo ya siku tano yaliyoendeshwa na Bodi ya Korosho Tanzania kwa Maafisa ugani hao leo Januari 17,2025 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg.Francis Mkuti amesema kuwa.mafunzo hayo yamewapa.mwanga zaidi ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwenye maeneo waliyopangiwa.
Aidha amewasistiza kutunza na kutumia kwa usahihi vitendea kazi watakavyokabidhiwa sambamba na kuimarisha ushirikiano na viongozi watakaowakuta kwenye maeneo waliyopangiwa ili kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Ndg.Francis Alfred amewasistiza kuzingatia maadili,ushirikiano na nidhamu katika utekelezaji wa shughuli zao ." Tunaimani mafunzo haya yatakuwa chachu ya kutekeleza majukumu yenu ipasavyo zingatieni maadili,ushirikiano na nidhamu ili kufikia malengo, sisi tupo nanyinyi kutoa ushirikiano lengo tufikie kiwango cha uzalishaji wa zao la Korosho,"
Maafisa ugani hao wameshuru na kuipongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo wameahidi kujituma na kushirikiana na wlae waliopo ili kufikia malengo.
#Tandahimba tumejipanga kazi zinaende
lea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa