• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Tandahimba yatoa eneo kwa ajili ya Ujenzi wa Kiwanda na Ghala

Posted on: April 8th, 2020

Na Kitengo Cha Habari na Mawasiliano

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka  ametoa eneo kwa ajili ya Mtandao  wa kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) kujenga kiwanda na ghala la kisasa kwa  ajili ya wakulima wa korosho

Akizungumza  ofisini kwake Msomoka amesema kuwa kiwanda  kitakachojengwa kitawasaidia wakulima kuweza  kuuza korosho zao ambazo zimebanguliwa na ambazo bado kwa kuwasogezea huduma

“Tunawakaribisha katika Wilaya  yetu na tunawapa eneo kwa ajili ya kiwanda na ghala kwasababu tunajua kitakuwa msaada mkubwa kwa wakulima wetu,hata hivyo tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza Tandahimba maeneo yapo  kwa ajili ya uwekezaji,”amesema Msomoka

Aidha amesema kuwa   mbali na ujenzi  huo Mkikita  wanatarajia kuboresha thamani ya korosho kwa kutoa pembejeo na  mbinu mbalimbali kwa wakulima ambapo wanatarajia kuingia mkataba na Umoja wa wakulima korosho Tandahimba(Uwokota) na Kitama Farmers

Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi (Mkikita) Adam Ngamange amesema kuwa lengo ni  kuongeza thamani ya zao la korosho sambamaba na kuwashawishi wawekezaji wa viwanda na kufungua kliniki ya kilimo  ya mazao mbalimbali



“Lengo la mtandao wetu wa kijani kibichi  ni pamoja na kuongeza thamani ya korosho ,kujenga kliniki ya kilimo kwa mazao mbalimbali ,kutoa mafunzo yanayohusu kilimo sambamba na kuwapa mitaji,pembejeo ,ushauri kuhusu mazao na kutafuta  masoko,”amesema Ngamange

Hata hivyo naye Mwenyekiti wa  Umoja wa wakulima korosho Tandahimba(Uwokota) Shabia Kajete amesema uwekezaji huo utawasaidia wakulima kupata  huduma bora karibu yao

“Mtandao huu ukijenga kiwanda na ghala utatusaidia sisi wakulima kwakuwa wakulima wengine wanabangua korosho zao lakini wanakosa mahali pa kupeleka  korosho hizo lakini sasa hivi watapunguza tatizo hilo kwa wakulima,”amesema Kajete 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa