• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

DC awataka wananchi Tandahimba kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

Posted on: March 16th, 2020

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Benaya Kapinga  amewataka wanannchi  kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona kwa kuacha kusalimiana kwa kushikana mikono na kuchukua  tahadhari  dhidi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia Wilaya ipo karibu na nchi jirani

Akizungumza kwenye kikao cha ufunguzi wa taarifa fupi ya Ugonjwa wa Corona katika Wilaya ya Tandahimba Kaimu Dc  ametoa maagizo kwa taasisi zote  ambazo zipo ndani ya Halmashauri ya Tandahimba kuweka maji ya kunawia mikono tiririka  ili kila anayeingia aweze kunawa mikono ikiwa ni hatua za awali za kujikinga na maambukizi


Kaimu Dc Benaya Kapinga akifungua kikao cha taarifa fupi ya Ugonjwa wa Corona  Wilaya ya Tandahimba

“Kwa kupitia kikao hiki  tunagiza  taasisi zote ndani ya Wilaya ya Tandahimba waweke maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono kwa kila  mtu atakayetaka huduma yoyote , shuleni na nyumbani yawekwe maji  ili kujikinga na maambukizi haya,”amesema Kapinga

Aidha amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu pia katika nyumba za ibada sambamba na kuacha kusalimiana kwa kupeana mikono badala yake tahadhali za awali zichukuliwe hasa katika mikusanyiko  ya watu


Wajumbe walioshiriki katika kikao hicho  leo wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai

Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela  ameeleza kuwa Halmashauri tayari imetenga fedha kwa ajili ya kuwezesha Kitengo cha afya kupata vifaa vya kupima joto la mwili hususan katika maeneo  ya mipakani

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Ally Machela(aliyesimama) akifafanua jambo 

“Hii ni dharura nasisi tunapakana na nchi jirani  kwa vile mipaka hii inapitisha raia wa kigeni kifaa cha kupima joto mwili katika mipaka yetu ni muhimu hivyo tunajitahidi  kukipata kwa haraka ili kuweza kupimia wagonjwa badala ya kipimo cha kuweka kwapani kutokana na hali iliyopo sasa,”amesema Machela

Naye Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Tandahimba Dokta Antpas Swai amesema  wananchi waendelee kuchukua tahadhari  ili kujikinga na maambukizi ya Corona

Amesema kuwa tayari Wilaya imetenga  Zahanati ya Mtegu kwa ajili ya dharura  endapo atapatikana mgonjwa wa corona sambamba na maandalizi ya vifaa kwa timu ambayo itashughulikia wagonjwa hao

Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Antpas Swai

“Tumejiandaa tayari kama Hospital ya Wilaya tumetenga zahanati ya Mtegu kwa atakayedhibitika kuwa nao,lakini pia wale ambao tutawahisi pia tumetenga eneo nje ya Hospital ya Wilaya  kwa ajili ya watakaosubiri majibu  baada ya kuonesha dalili za awali,”amesema Dk Swai

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa