UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ni moja kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Mtwara. Ina eneo la 167,331Ha. Kwa upande wa Magharibi imepakana na Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Mashariki imepakana na Wilaya ya Mtwara Vijijini na upande wa kaskazini imepakana na mto Ruvuma mpaka rasmi wa Tanzania na Nchi ya Msumbiji. MUUNDO WA UTAWALA
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imegawanyika katika Tarafa tatu za Litehu, Mahuta na Namikupa. Pia Wilaya ina kata 31, Vijiji 143, Mitaa 14 na Vitongoji 654 na Jimbo moja la uchaguzi. Kuanzia tarehe 1/07/2015 Halmashauri ya Tandahimba imepata Mamlaka mbili za Miji Midogo ya Mahuta na Tandahimba
IDADI YA WATU
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 yenye ongezeko la watu wastani wa 1.2 kwa mwaka,katika mwaka 2016 Wilaya inakadiliwa kuwa na watu 238,632 ikiwa wanawake ni 128,053 na wanaume 110,579. Kulingana na ongezeko hilo la 1.2 kwa mwaka 2016 Wilaya inakadiliwa kuwa na wastani wa kaya 64,495 zenye wastani wa watu 3.7 kwa kaya
SHUGHULI ZAKIUCHUMI.
Kilimo Shughuli kuu za kiuchumi zinazofanywa na wakazi wa Tandahimba Wilaya ni kilimo cha mazao na ufugaji. Korosho ikiwa ni zao kuu la biashara ikifuatiwa na mazao ya ufuta, muhogo,mbaazi, njugu na karanga. Mazao ya chakula ni pamoja na muhogo (chakula kikuu), Mtama, mahindi, mpunga na kunde.
Mifugo Kwa upande wa mifugo kuna ufugaji wa kuku, mbuzi, bata,kondoo, samaki n.k
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa