Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasistiza wasimamizi wa miradi ya Uboreshaji wa miundombinu ya ujifunzaji na na ufundishaji kwa shule za msingi (BOOST) kuzingatia mpango kazi sambamba na miongozo iliyotolewa katika utekelezaji wa miradi hiyo kwenye maeneo yao husika
Akizungumza Aprili 19,2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmasahauri na wadau wa maeneo ambayo miradi hiyo itatekelezwa Dc Sawala amesema kuwa kikao hicho cha kujenga uelewa kwa wadau kitaleta ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya BOOST kwa wakati
" Tunamshukuru Mhe Rais kwa juhudi anazofanya za maendeleo ,muhimu hakikisheni mnaisimamia na kuifuatilia miradi ili iweze kukamilika kwa wakati,viwango na ndani ya bajeti iliyotolewa,zingatieni mpango kazi ambayo itakuwepo katika maeneo yenu ya miradi"amesema Dc Sawala
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amesema lengo la kikao hicho ni kujenga uelewa wa miradi ya BOOST kwa wadau hao ambapo kwa awamu ya kwanza kiasi cha fedha shilingi Mil.665.1 zitatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo
" Wakati wowote kuanzia sasa tutapokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya BOOST ,ninaamini miradi hiyo itakavyotekelezwa kwa ufanisi na maelekezo yake yatazingatiwa ili tuweze kuendelea kupata fedha hizo kuboresha miundombinu ya elimu msingi katika Halmashauri yetu, "amesema Mkurugenzi
Aidha amesema kwamba fedha hizo zitatekeleza miradi katika shule za msingi saba(7) ambazo ni Amani,Chikongola,Michenjele, Mjimpya,Mihambwe na Mambamba ambapo itajengwa shule mpya ya kisasa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa