Na Kitengo cha Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipokea fedha Tsh.156,250,000 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya umaliziaji wa maboma 13 ya madarasa ya shule ya msingi ambapo maboma 12 yamekamilika na moja (1) lipo hatua za mwisho za umaliziaji
Gharama ya kila Boma ni shilingi milioni kumi na mbili na laki tano (12,500,000) ambapo fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti za shule husika
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba tunamshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizo ambapo zimeboresha miundombinu ya shule zetu za msingi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa