Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Kiasi cha zaidi ya milioni 279 zimetumika kwenye zoezi la malipo ya mwezi Novemba na Disemba kwa walengwa wa kaya maskini 6220 Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kati ya walengwa 6242
Mratibu wa TASAF Tandahimba Ismaely Mbilinyi
Akitoa tathmini hiyo Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi amesema kuwa zoezi hilo la siku tano limewafikia walengwa kwenye vijiji 88
“Zoezi limekamilika kiasi cha shilingi 279,452,000 zimetumika kukamilisha zoezi hili kwa walengwa wa Halmashauri yetu kwa vijiji 88,”amesema Mratibu
Afisa Ufuatiliaji wa TASAF Tandahimba Faida Mabele akizungumza na wanufaika wa kaya maskini wakati wakisubiri malipo
Aidha katika zoezi hilo kaya 22 hazikushiriki katika zoezi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo,baadhi yao kufuzu na wengine kutokuwepo katika maeneo yao wakati wa zoezi la malipo hivyo kiasi cha shilingi milioni sita hazikuweza kulipwa kwa walengwa hao
Mratibu amesema moja ya changamoto ambazo zimejitokeza katika zoezi la malipo kwa mwezi Novemba na Disemba ni pamoja na baadhi ya majina kutokuwepo kwenye orodha,kuchelewa kwa malipo na ukosefu wa vitambulisho vipya kwa baadhi ya walengwa
Wanufaika wa kaya maskini wakisubiri malipo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa