Na Kitengo cha Mawasiliano
Wito umetolewa kwa.Wajumbe wa Kamati ya Afya ya msingi ya Wilaya ya Tandahimba kutimiza wajibu wao kwenye nafasi zao ili malengo ya Kampeni ya Kitaifa ya utoaji wa chanjo ya Surua Rubella yatimie.
Akizungumza leo Februari 14,2024 kwenye kikao cha Kamati ya afya ya Msingi ya Wilaya kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ,Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Ndg.Francis Mkuti amesema kuwa kila mjumbe akatimize wajibu wake wa kuwajengea uelewa wananchi kuhusu kampeni hii.
Naye Kaimu Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi. Joselyne Kalikawe akitoa wasilisho kwa Kamati ya Afya Msingi ya Wilaya ameeleza kuwa ugonjwa wa Surua na Rubella huenezwa kwa njia ya hewa,hivyo chanjo hiyo itasaidia kumkinga mtoto kuanzia miezi tisa hadi chini ya umri wa Miaka mitano na magonjwa hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeweka lengo la kutoa chanjo hiyo kwa watoto 30632 kwenye Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua Rubella ambayo inaanza rasmi kesho Februari15-18,2024 ambapo huduma hiyo itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya,shuleni,sokoni na maeneo yaliyotengwa.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa