Na Kitengo cha Mawasiliano
Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uelewa ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akifungua mafunzo hayo ya Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji leo Desemba 16,2024 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mwl.Sosthenes Luhende amewasistiza kuzingatia mafunzo hayo ili kutekeleza majukumu ya.kila siku kwenye maeneo yao .
kwa upande wa wawezeshaji wamewasilisha mada mbalimbali ikiwemo Uendeshaji wa vikao na mikutano katika ngazi ya Vijiji,Mitaa na Vitongoji,Uibuaji,Upangaji na usimamizi wa Miradi shirikishi ya jamii,Usimamizi na udhibiti wa fedha katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Uongozi na Utawala bora.
Naye Mhe.Karimu Mtimbuka Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanhyanga C akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa vijiji na vitongoji amesema mafunzo hayo yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao na kuipongeza Serikali kwa hatua hiyo ya kuona umuhimu wa kupatiwa mafunzo ili kuwajengea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa