Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala ameagiza hatua za kisheria zichukuliwe kwa wazazi watakao kaidi agizo la kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda Shule na waliokatiza masomo kwa Utoro wanahudhuria Shuleni mara itakapofunguliwa ili kupata Elimu ambayo ni haki yao ya Msingi
DC Sawala ameyasema hayo leo Septemba 8,2023 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mihambwe ambapo amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi sambamba na kutoa maelekezo ya Serikali
"Serikali imeendelea kuboresha Miundombinu ya Elimu kwa kujenga Madarasa ya kutosha ili Wanafunzi wasome katika Mazingira bora,hivyo wazazi hakikisheni wanafunzi waliokatisha masomo kwa utoro wanakwenda shule, ni haki ya Msingi kwa watoto kupelekwa Shule na kuhakikisha wanahitimu masomo ili kufikia malengo yao," amesema DC Sawala
Miongoni mwa kero zilizoanishwa ni pamoja na Wananchi kutaka kujua bei elekezi ya Korosho Msimu huu 2023/2024 suala ambalo amelitolea ufafanuzi kuwa bei itatangazwa rasmi muda ukifika huku akisisitiza wananchi kupeleka na kuuza Korosho kwa Mfumo wa Stakabadhi ghalani Msimu wa mauzo utakapofika
Aidha katika suala la Pembejeo Wananchi wa Kata ya Mihambwe wameishukuru Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Pembejeo za ruzuku kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa