Waumini wa dini ya Kiislamu Wilaya ya Tandahimba wamefanya dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ikiwa ni shukrani yao ya kuwapatia Fedha Shilingi Milioni Mia Moja(100,000,000) kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Msikiti wa Wilaya.
Dua hiyo immefanyika leo Februari 8,2025 kwenye Uwanja wa Msikiti wa Wilaya ikiongozwa na Sheikh wa Wilaya ya Tandahimba Salum Ismail Njapuka na kuhudhuriwa na Viongozi wa Serikali,Masheikh wa Kata na Waumini wa Dini ya Kiislamu.
Naye Katibu Tawala Ndugu Rashidi Shabani Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba amewapongeza kwa kuandaa dua hiyo ya kumuombea Mhe.Rais lakini pia amewasistiza Uongozi wa Msikiti kutumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa ili waumini wapate sehemu ya kuabudu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema Mhe.Rais amewatendea wana Tandahimba wema ambao hawataweza kuulipa zaidi ya kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda
" Tunawashukuru Uongozi wa Bakwata Wilaya kwa kuandaa Dua maalum kwa ajili ya Rais wetu,Kwa wema aliotufanyia hatuna cha kumlipa zaidi ya dua ili Mwenyezi Mungu aendelee Kumlinda Rais wetu ,"amesema Mwenyekiti
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa