Na Kitengo cha Mawasiliano
Watoa huduma wa afya ngazi ya Jamii (WAJA) Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba wamesistizwa kuendelea kutoa elimu ya afya na lishe katika maeneo yao
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Aloyce Massau kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amewasistiza WAJA kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuboresha afya na lishe katika jamii
Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 29,2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo wawezeshaji wamewasilisha mada ya Siku ya afya na lishe ya kijiji,makundi matano ya vyakula,ulishaji wa watoto wachanga na wadogo, na umuhimu wa unyonyeshaji ambazo zitaongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao kwenye ngazi ya jamii
Aidha WAJA wamesistizwa kutoshiriki kupima uzito wa watoto katika vijiji bila kuwa na mtoa huduma za afya kwenye eneo husika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa