Na.Kitengo cha Mawasiliano
Zaidi ya watoa huduma za Afya Tisa kwenye vijiji vilivyo mbali kwa Kilomita 5 kutoka eneo la kituo cha kutolea huduma za Afya wamepewa vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kurahisisha utekelezaji wa Majukumu yao.
Akigawa vifaa hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Francis Mkuti amesema Serikali imeendelea kuboresha huduma za Afya na kuhakikisha kila Mwananchi anapata huduma hiyo popote alipo.
Aidha, Mkuti amewasisitiza wataalamu hao kuvitumia vyema vifaa hivyo ili vilete tija katika kuwahudumia Wananchi.
Awali akitoa taarifa ya Vitendea kazi Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dkt. Adorat Mpollo amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Baiskeli , Mizani , Kipimajoto ,Stop watch ,Simu Janja na Vishikwambi ambavyo vyote vitawasaidia iwapo Kuna mgonjwa Yuko eneo la Kijiji waweze kumfikia haraka na kumpatia huduma ya Afya.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa