Na Kitengo cha Mawasiliano.
Timu ya wataalamu, Waheshimiwa Madiwani na Mheshimiwa Mbunge kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru wamefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Leo Machi 4, 2024 kwa ajili ya kujifunza zao la Korosho na uuzaji wa Mazao kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani.
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imekuwa ikifanya vizuri katika uuzaji wa Mazao yake kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani ikiwemo Korosho, Ufuta na Mbaazi.
Wageni hao wamepokelewa na Viongozi wa Wilaya ya Tandahimba akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Kanali Patrick Sawala, Mkurugenzi Mtendaji ACI.Mariam Mwanzalima pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Baisa Baisa.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa