Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka Watendaji Kata kuwashirikisha wazazi na walezi kuchangia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno
Amesema hayo Mei 15,2023 katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe robo ya tatu 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, ambapo Dc Sawala amesema kuelekea kipindi cha mavuno wazazi na walezi washirikishwe ili waweze kuchangia chakula cha mwaka mzima
" Watendaji Kata mkasimamie wazazi na walezi kipindi hiki tunachoelekea cha mavuno wachangie chakula ili wanafunzi wote wapate chakula ,ni rahisi mzazi kuchangia kipindi hiki ambapo anavuna mazao mbalimbali,mkatumie nafasi hii kuwashirikisha lakini pia mkahakikishe chakula kinachopatikana kinahifadhiwa vizuri ," amesema Dc Sawala
Aidha amewapongeza Watendaji Kata kwa kuendelea kutekeleza afua za lishe katika maeneo yao pia amewasistiza kusimamia na kufuatilia maazimio waliojiwekea ya kufikia lengo la asilimia 100 kwa viashiria vyote katika kila Kata
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa